UJUMBE WA BABA MT. YOHANE PAULO II -- JUMAPILI YA ENEZO LA IMANI 2002 "UTUME NI KUTANGAZA MSAMAHA" NDUGU ZANGU WAPENDWA, 1. Kazi ya Utume wa Kanisa ni hasa kutangaza upendo, huruma na msamaha wa Mungu, vilivyoletwa kwetu kwa njia ya maisha, kifo na ufufuko wa Yesu Kristu Bwana wetu. Ni kutangaza habari njema ya kwamba Mungu anatupenda na anataka watu wote walioungana katika huruma yake ya Upendo anatusamehe na anatutaka kuwasamehe wengine hata kama wamekosea kwa kiasi gani. Hili ndilo neno la upatanisho tulilokabidhiwa asemavyo Mt. Paulo: Mungu alipata kuhesabu uovu wa mwanadamu na akamkabidhi ujumbe wa upatanisho kwetu, "Yaani Mungu alikuwa ndani ya Kristu, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake asiwahesabie makosa yao; naye anletia ndani yetu neno la upatanisho" (2Kor 5:19). Maneno haya ni mwangwi na yanatukumbusha kilio kikuu kutoka katika Moyo wa Kristu msalabani, Yesu akasema "Baba, uwasamehe kwani hawajui watendalo" (Lk 23:34). Kwa ufupi, haya ndiyo mambo muhimu yahusuyo Jumapili ya kuombea huduma ya uenezaji Injili tutakauoadhimisha jumapili tarehe 20 Oktoba 2002, yenye mada ya kuchangamsha, "Utume ni kutangaza msamaha". Ingawa tukio hili hufanyika kila mwaka, lakini kwa kadiri tunavyosonga mbele nyakati hazipotezi chochote kinachohusu umaana na umuhimu wake, kwani utume ni mwitikio wetu kwa Amri Kuu ya Yesu, "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu" (Mt. 28:19) 2. Mwanzoni mwa milenia ya tatu jukumu la kimisionari ni muhimu zaidi, kwa sababu, kama nilivyosema katika barua ya kipapa ya "Redemptoris Missio", (utume wa mkombozi) idadi ya wasiomjua Kristu na ambao sio wanakanisa inazidi kuongezeka, kwa kweli kutoka mwisho wa mtaguso idadi hiyo imekuwa ni mara mbili zaidi. Tukiangalia sehemu hii kubwa sana ya binadamu hao wanapendwa na Baba na ambao kwa ajili yao alimtuma mwana wake, swala la utume wa Kanisa ni dhahiri na ni muhimu sana na la haraka, (N° 3). Pamoja na mtume mkuu na mwinjilishaji Mtakatifu Paulo nasi tunapenda kurudia, "Hata hivyo kuhibiri Injili ni jambo la kutambia, ni jukumu hivyo sina uchaguzi binafsi. Ole wangu nisipotangaza Injili, ni wajibu kwangu" "Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina lakujisifia; Maana nikitenda kazi hii kwa hiari yangu ninathawabu ila ikiwa is kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili" (1Kor. 9:16-17). Ni upendo wa Mungu pekee unaoweza kuwaunganisha watu wote, wa kutoka kila kabila na tamaduni mbalimbali kunaweza kutibu kila aina ya magomvi ya kiitikadi, uchumi usioungana na utumiaji nguvu, utengano unaoumiza, ambao bado unamkandamiza binadamu. Wote tunaelewa juu ya vita za kutisha na mapinduzi yaliyoijaza damu karne iliyopita na magomvi ambayo kwa bahati mbaya bado yanaendelea kuukumba ulimwengu kwa kasi. Hata hivyo haiwezi ikafumbiwa macho jinsi ongezeko la watu duniani wanaume kwa wanawake ambao licha ya umaskini mkubwa wa kiroho na kimwili, wanakiu kubwa ya Mungu na huruma yake ya upendo. Wito wa Bwana wa kuhubiri habari njema ni bado unahitajika na kwa kweli hasa wakati huu ni muhimu zaidi. 3. Katika barua kitume 'NIVO MILLENNIO Ineunte' nimesisitiza umuhimu wa kutafakari sura ya Yesu Mteswa na Mtukufu kiini cha ujumbe wa Kristu ni kutangaza Fumbo la Pasaka ya Kristu aliyesulubiwa na aliyefufuka. Tukitafakari uso wa msulubiwa katika kilele cha mateso makali, "Tumeona mbele yetu siri kuu ya upendo wake ikijitokeza katika sala yake ya mwisho pale msalabani" (N. 25). Mungu ametufunufia sisi sote siri kuu ya upendo wake pale Msalabani. Msalaba ni ufunguo ambao unaruhusu kuingia katika "Hekima ambayo si ya ulimwengu huu, wala si ya watawala wa enzi tusemavyo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatitika; bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu." (1Kor. 2:6-7). Msalaba ambamo uso wa Kristu Mfufuka tayari unang'aa, unatuingiza katika utimilifu wa maisha ya kikristu na upendo kamili, kwani unadhihirisha tamaa ya Mungu ya kuwashirikisha wanadamu maisha yake, upendo wake, utakatifu wake. Katika nuru ya fumbo hilo hilo kama likikumbuka maneno ya Bwana. "Muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyomkamilifu" (Mt. 5:48) linaeleweka wazi zaidi kwamba utume wake utakuwa hauna maana iwapo hautaelekea kwenye utimilifu wa maisha ya kikristu, yaani upendo kamili wa utakatifu. Kwa kutafakari Msalaba tunajifunza kuishi unyenyekevu na msamaha, amani na ushirika. "Huo ndio uliokuwa uzoefu wa Mt. Paulo anayewaandikia Waefeso, "Nalia pamoja nanyi "Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mtioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani" (Efe 4:1-3). Na pia kwa Wakorintho anaongezea : "kwa sababu kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamni, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. Kazi ya mtu aliyojenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mweneywe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto." (1Kor 3:12-15). 4. Wapendwa sana ndugu zangu kilio cha Yesu msalabani "Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti uake kwa nguvu aksiema, "Eloi, Eloi, lama sabakthani?" yaani, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?" (Mt 27:46) si ishara ya mtu aliyekata tamaa, bali ni sala ya Mwana anayekabidhi uhai wake kwa Baba yake kwa ajili ya wokovu wa watu wote. Kutoka msalabani Yesu ametuonyesha masharti yanayotuwezesha kusamehe kwa ile chuki ambayo kwa wale watesi wake waliompigilia Msalabani, anajibu kwa sala ya kuwaombea. Na haishii kuwaombea tu, bali anaendelea kuwapenda, kuwatakia yote mema, anawaombea, kifo chake kinakuwa ni utekelezaji kamili wa upendo. Hivyo mbele ya fumbo hili kuu la msalaba tunaweza tu kupiga magoti na kuabudu. "Ili kumrudisha mwanadamu mbele ya uso wa Baba, Yesu Kristu hakuchukua tu sura ya mwanadamu bali alitwaa pia mzigo wa "sura" ya dhambi. "Kwa ajili yetu alimfanya awe dhambi yaye aliyekuwa hana dhambi, ili katika yeye tuweze kuhesabiwa haki." "Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye." (2Kor.5:21), NOVO MILLENIO Ineunte, 25). Msamaha kamili wa Yesu, hata kwa watesi wake, ni mwanzo wa haki mpya itokayo katika ufalme wa Mungu kwa ajili ya kila mtu. Katika karamu ya mwisho, Yesu aliwaambia Mitume wake, "Nawapeni amri mpya Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watawatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi." (Yn 13:34-35). 5. Kristo mfufuka anawapa amani wafuasi wake. Kanisa likuwa aminifu kwa amri ya Bwana, linaendelea kutangaza na kueneza amani yake. Kwa njia ya uinjilishaji, waamini wanawasaidia wengine kutambua kuwa sote tu ndugu, kama wasafiri katika dunia hii, hata kama kwa njia tofauti za maisha, sote tupo njiani kuelekea nyumbani ambapo Mungu, kwa njia zijulikanazo na yeye tu hachoki kutuonyesha. Njia kuu ya utume ni uwazi katika mazungumzo, na (Ad Gentes 7, Notra aetate 2) mazungumzo hayazuiliwi na mbinu bunifu za ubinafsi (RM 56) wala siyo lengo la walengwa wa Mazungumzo kumbe yanasemwa na wengine kwa heshima, kuelewa na kutaja hoja tunazosadiki na kutangaza kwa upendo, ukweli wa ndani wa imani ambao ni furaha, tumaini na maana halisi ya maisha. Kwa kweli mazungumzo ni utekelezaji wa msukumo wa kiroho unapelekea uongovu ambao ukitafutwa kwa unyofu, kwa utakaso wa ndani, Roho Mtakatifu huzaa matunda ya kiroho (Tor. Juu 59). Kujitoa kwa mazungumzo ya uangalifu na kuheshimiana (conditio) sine qua non) (sharti ambalo bila hilo hakuna) ni kiini na ushuhuda wa kweli wa pendo la wokovu wa Mungu. Mazungumzo haya yanaambatana kwa karibu na utayari wa kusamehe, kwa sababu mtu anayesamehe anafungua mioyo ya wengine na anajifunza kuwapenda na kuwaelewa wengine akiingia katika mapatano na wengine. Kwa sababu kitendo cha kusamehe, kwa kufuata mfano wa Yesu, kinatoa changamoto, kinafungua moyo, kinaponya madonda ya dhambi, utengano na kinajenga ushirika wa kweli. 6. Kuadhimisha Jumapili ya Umisionari, kunatoa kwa kila mmoja fursa ya kujitafiti juu ya mahitaji ya upendo usio na mwisho wa Mungu. Upendo unaotaka imani, upendo unaotuambia tuweke matumaini yetu yote kwake. "Bila imani "Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba Yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao" (Ebr. 11:5). Katika tukio la mwaka huu tunaalikwa kusali kwa nguvu kwa ajili ya misioni na tuchangie kwa kila njia katika kazi za Kanisa duniani kote ili kujenga ufalme wa Mungu," ufalme wa milele na wa dunia nzima, ufalme wa kweli na uhai, ufalme wa utakatifu na neema, ufalme wa haki, upendo na amani" (Tor. Utangulizi wa sikukuu ya kristu mfalme). Tunaalikwa kutoa ushuhuda kwanza kabisa kwa njia ya maisha yetu kujitoa kabisa kwa Kristu na Injili yake. Ndipo lazima tusiionee aibu Injili na tusiogope kujitangaza kuwa sisi ni Wakristu, kwa kuficha imani yetu. Badala yake lazima tuendelee kusema na kupanua mazingira kwa ajili ya kutangaza wokovu, kwa sababu Yesu ametuahidi kuwa pamoja nasi daima na yupo pamoja na mitume wake. Jumapili ya umisionari, sikukuu ya umisionari, inatusaidia kugundua thamani ya wito wetu kama mtu binafsi, na kama jumuiya. Inatuamsha kuwafikia "ndugu zangu walio wadogo". "Na mfalme atajibu, akiwaambia, 'Amini, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. (Mt. 25:40). Kwa njia ya wamisionari popote duniani. Huu ni wajibu wa vyama vya kipapa vya kimisionari, ambayo daima vimekuwa tayari kuhudumia utume wa Kanisa, kuhakikisha kwamba wale walio wadogo kabisa hawakosi kuwa na wale wanaomega nao mkate wa neno, wanaoendelea kuwaletea zawadi ya upendo wa Mungu usio na mwisho unaobubujika katika Moyo wa Mkombozi wetu. Wapendwa sana ndugu zangu, hebu tukabidhi kazi hii ya kuitangaza Injili na hasa shughuli zote za uinjilishaji katika Kanisa mikononi mwa Bikira Maria, Malkia wa shughuli za misioni. Tumwombe aongozane nasi katika safari ya kushuhudia upendo wa Mungu anayesamehe na anayetoa amani kwa watu wote. Kwa hisia hizo kwa wamisionari wote duniani, kwa wote wanaowasindikiza kwa njia ya sala na misaada mbalimbali ya kidugu, kwa jumuiya za kikristu, za zamani na miundo mipya, kwa furaha natoa baraka yangu ya kitume nikiwaombea ninyi nyote ulinzi wa Bwana daima. Imetolewa Vatikani, Mei 19, 2002 Sikukuu ya Pentekoste Yohanne Paulo II 3 C:\Documents and Settings\Administrator\My Documents\My Webs\MaryknollAfrica.org\Documents\Pope's Message for World Mission Sunday 2002 - Swahili.doc 3